Taarifa Juu Yetu

Kitabu kitakatifu cha Kikristo kinatueleza vyote viwili, historia na unabii. Kinatueleza kilichowahi kutokea na kitakachotokea hivi karibuni. Katika utabiri wa kustaajabisha, twaweza kusoma ujumbe wa mwisho wa tahadhari kabla ya kuangamizwa kwa ulimwengu.

Ujumbe huu wa tahadhari, ulioelezwa na Malaika Watatu wa Ufunuo 14, unakuja katika vipengele vitatu. Kila kipengele cha ujumbe huu ni cha muhimu sana kwa ulimwengu wote kukisikia.

  • Malaika wa kwanza anatueleza kumwabudu Mungu Muumba, Yeye aliyeziumba mbingu, nchi, na bahari. Tunapaswa kumwabudu Muumba kwa sababu saa ya hukumu Yake imewadia. Malaika wa kwanza anatuambia jinsi tunavyoweza kumjua Mungu huyu na kujiandaa kushinda katika hukumu.

  • Malaika wa pili anatutahadharisha juu ya uasi wa kidini katika wakati wa mwisho. Tunaambiwa 'tutoke' katika mifumo ya dini ambayo haimheshimu Mungu Muumba na Neno Lake lililofunuliwa.

  • Malaika wa tatu anatuonya kuwa yule mwovu atafanya kazi kupitia mfumo wa kidini ulioasi kuandaa shambulizi moja la mwisho kwa Mungu na watu Wake. Kutakuwa na 'alama' iliyowekwa kwa wale wanaomfuata yule mwovu, na wale wanaoendelea kuwa waaminifu kwa Mungu watateswa. Lakini Mungu atamimina hukumu Zake juu ya wote wenye alama hii ya kutisha. Watu wake walio na imani na utii, wataokolewa kutoka kwenye majonzi ya dunia hii inayoangamia. Wataenda mbinguni na Mungu, nao wataangalia wakati Mungu Akiumba upya dunia katika ukamilifu wake wa awali.

Jisajili kwa ajili ya jarida letu

Kuwa wa kwanza kujua pale machapisho mapya yanapotoka

newsletter-cover