
Mwito wa Kuhama
Muhtasari
Je, una shauku ya mahali bora zaidi? Mahali pa usalama, furaha, na pumziko? Tunashauku ya kitu ambacho hatuwezi kukipata hapa ulimwenguni kwa kuwa kila mmoja wetu aliumbwa kwa ajili ya Paradiso. Yesu aliye Masihi tayari amekwenda huko. Anaijua njia, na hakika, Anasema kuwa Yeye ndiye "Njia!" Kitini hiki kinaelezea ukweli muhimu juu ya Yesu ambao unatusaidia kujitayarisha kwa ajili ya uraia kule Paradiso.
Aina
Kijitabu
Mchapishaji
Sharing Hope Publications
Inapatikana katika
38 Lugha
Kurasa
6
Abdul-Malek alikuwa mzee mnyong’onyevu. Baada ya kufiwa na mke na watoto wake, alikuwa ameikimbia Iraki ili kijinusuru na kikundi cha ISIS. Sasa alikuwa akiishi peke yake kule Jordan kama mkimbizi.
Lakini kulikuwa na dalili ya matumaini. Alikuwa na binamu yake anayeishi Kanada ambaye aliahidi kumsaidia kupata ajira. Akiwa amejawa na furaha, alituma maombi ya kupata viza na kuanza kupata njozi juu ya maisha rahisi zaidi. Hatimaye, baada ya miaka mingi ya kungoja, alipata kibali cha kuingia nchini Kanada. Abdul-Malek alifurahi sana!
Lakini furaha yake ilidumu muda mfupi tu. Baada ya kuwasili nchini Kanada, aligundua kuwa maisha baada ya kuhamia pale si rahisi. Kazi yake ilimshughulisha siku nzima. Majirani zake walikuwa ni wenye kupiga kelele. Usafiri wa umma haukuwa rahisi kuuelewa—kadhalika na lugha ya Kiingereza!
Abdul-Malek siku zote alikuwa na njozi ya kwenda mahali pazuri zaidi, lakini mara alipowasili, aligundua kuwa moyo wake bado ulikuwa unauma. Alianza kujiuliza kama shauku aliyokuwa nayo ingeweza kukidhiwa na mahali popote maalum hapa duniani—au kama ingembidi kusubiri mpaka Paradiso yenyewe!
Kuhamia Paradiso
Je umewahi kujisikia kama Abdul-Malek? Shauku hii kwa ajili ya mahali palipo pazuri zaidi imo ndani ya moyo wa mwanadamu na inaweza tu kukidhiwa kwa kuingia Paradiso, nyumbani kwetu halisi. Nayo ni shauku ambayo itatimizwa muda si mrefu! Ishara za Saa ile zinatimilika mbele za macho yetu, na dunia hii inafikia mwisho wake punde.
Kwa karne nyingi, vitabu vya kidini vya Wayahudi, Wakristo, na Waislamu vyote vimetabiri juu ya kiyama—kile kilele cha juu kabisa wakati “tutakapohama” kutoka katika ulimwengu huu na kuingia katika ule unaokuja. Imani zote tatu huelekeza kwa mtu mashuhuri aitwaye Masihi ambaye atawajibika na utimilifu wa matukio haya ya mwisho.
Cha kuvutia, mtu huyu Masihi katika Ukristo na Uislamu si mwingine bali ni Yesu Kristo, ambaye pia anafahamika kama Isa al-Masih. Alikuwa ni Masihi alipoishi kule Palestina, lakini amekuwa akiishi katika Paradiso kwa zaidi ya miaka 2,000 iliyopita. Hatimaye atarudi katika Siku ya Mwisho ya Hukumu.
Kurudi kwa Yesu Kristo kunatajwa mno katika Biblia, lakini Waislamu pia wanaamini kuwa anakuja tena, kwa vile imeandikwa katika Kurani: “Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka” (Azzukhruf 43:61).
Kama vile afisa wa uhamiaji anavyotoa mwongozo muhimu juu ya namna ya kupata viza, Yesu Kristo anatualika kuzingatia Ishara Yake ili tuijue Njia iliyo Nyooka kwenda Paradiso.
Je, Yesu Alisema Paradiso Ikoje?
Vitabu vya Injili ambavyo hufahamika pia kama Injili vimeandika kuwa Yesu Kristo alisema, “Maana Naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo Mimi nanyi mwepo” (Injili, Yohana 14:2, 3).
Yesu Kristo anasema kwamba anaweza kutupeleka Paradiso!
Pia alidhihirisha mwonekano mzuri wa mara moja wa mahali hapo. Alisema kwamba
Wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu (Ufunuo 21:4).
Tutakuwa na makao ya kupendeza (Yohana 14:2).
Wanaume na wanawake makundi yote mawili watakuwa na hadhi na haki sawa (Gal. 3:28).
Umejaa nuru, haki, na furaha (Ufunuo 21:21–25).
Kwa hakika, hapa ndipo mahali mioyo yetu inapopaonea shauku!
Kwa Nini Yesu Kristo Anakuja Mara ya Pili
Lakini Mungu ametuma manabii na wajumbe watakatifu wengi. Kwa nini Yesu Kristo amechaguliwa kuja mara ya pili? Swali hili ni rahisi kujibiwa kwa kielelezo kile kile cha uhamiaji. Kwa kuwa kupata viza si jambo rahisi, watu wengi wanamwajiri mwanasheria, ambaye anajua namna ya kushughulika nalo. Kama tunaye kiongozi, tunaweza kutumaini kuwa atatusaidia.
Vivyo hivyo, Yesu Kristo ndiye pekee anayetokea mara ya pili kwa kuwa anajua njia ya kwenda Paradiso na anaweza kutuongoza kufika pale. Yeye Mwenyewe alidai, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima” (Injili, Yohana 14:6).
Kila nabii na mjumbe aliyetumwa na Mungu amefanya makosa na ilibidi aombe msamaha. Ila si Yesu Kristo. Hakuwa na dhambi katika miaka yote 33 aliyoishi duniani. Hii ndio maana alitwaliwa mara moja kwenda Paradiso.
Imetupasa kujifunza kutoka kwa Yesu Kristo, Yeye pekee Asiye na dhambi, jinsi ya kukidhi masharti ya kuingia Paradiso. Ni kwa njia hii peke yake tutakuwa na hakika kabisa ya kuingia pale. Ni jambo la kushukuru kuwa, tunaweza kujifunza kutoka katika kitabu chake, Biblia.
Kujiandaa kwa Marejeo ya Yesu Kristo
Je si jambo la kufurahisha kuwa unaweza kuwa na uhakika wa kuhama kwako kwenda katika mahali palipo bora? Unaalikwa kuwa raia wa ufalme wa Mungu wa utukufu kule Paradiso! Punde Yesu atakuja kutupeleka sote katika mahali pale pa kupendeza.
Je yawezekana kuwa unawafuata binadamu ambao wao wenyewe hawajui litakalowapata katika ile Siku ya Hukumu? Ukiwa na Yesu, huna sababu ya kuwa na mashaka. Mwombe Mungu akuongoze katika njia iliyo Nyooka ya Yesu Kristo. Unaweza kufanya ombi kama hili:
Ee Bwana, moyo wangu una shauku ya mahali palipo bora. Tafadhali niokoe pamoja na wapendwa wangu kutokana na shida za dunia hii. Ninaamini muda ni mfupi. Tafadhali nipatie mwongozo ili nipate kuingia mahali pazuri ajabu uliponiandalia. Amina.
Kama ungependa kupata nakala ya kweli ya Injili, tafadhali wasiliana nasi kupitia katika taarifa iliyopo nyuma ya karatasi hii.
Tafsiri ya Qurani kwa Kiswahili Imetafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani.Copyright @ 2023 by Sharing Hope Publications. Kazi hii yaweza kuchapishwa na kusambazwa kwa watu wengine bure pasipo kuomba idhini kwa makusudi yasiyo ya kibiashara.Swahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Jisajili kwa ajili ya jarida letu
Kuwa wa kwanza kujua pale machapisho mapya yanapotoka

Tafuta Hadhira Yako
Machapisho Yaliyoangaziwa
© 2023 Sharing Hope Publications